|
Article on other languages:
|
Amerika ya Kilatini ni jina la kutaja sehemu kubwa ya Amerika. Asili ya jinaAmerika ya Kilatini humaanisha kwa kawaida nchi za Amerika ambako lugha za Kihispania na Kireno pamoja na Kifaransa hutumiwa kama lugha rasmi au lugha ya watu wengi. Lugha hizi zote zimetokana na Kilatini na hujumlishwa kama "Lugha za Kirumi". Nchi za Amerika ya KilatiniKuna tofauti kuhusu ya namna ya kutaja nchi za Amerika ya Kilatini. Mara nyingi Amerika ya Kusini, Amerika ya Kati na Meksiko hutajwa hivyo kwa jumla. Lakini kuna nchi ndogo kama Guyana, Surinam na nchi za visiwani vya Karibi zinazotumia zaidi Kiingereza au Kiholanzi zisizo lugha za Kirumi. Nchi hizi wakati mwingini hujumlishwa pamoja ndani ya Amerika ya Kilatini lakini mara nyingi zinatazamiwa kuwa pekee kiutamaduni. Kiutamaduni hata sehemu ya Marekani ya Kusini yenye wasemaji wengi wa Kihispania ni karibu sana na Amerika ya Kilatini. Majimbo haya ya Marekani kama Texas na Kalifornia yalikuwa sehemu za Meksiko hadi karne ya 19. Historia na utamaduniKipaumbele cha lugha za Kirumi kimetokana na historia. Baada ya Kristoforo Kolumbus nchi hizi zilikuwa koloni ama za Hispania au za Ureno hadi karne ya 19. Wakazi wengi ni watoto wa wahamiaji kutoka Ulaya au chotara kati ya wahamiaji wale na wakazi asilia. Katika nchi kadhaa hasa Meksiko na nchi za Andes ambako wakazi Waindio wengi kidogo walibaki wanaoendelea kutumia lugha zao pamoja na Kihispania. Dini kubwa katika Amerika ya Kilatini ni Kanisa Katoliki lililokuwa kanisa rasmi ya Hispania na Ureno. |
This article is from Wikipedia. All text is available under the terms of the GNU Free Documentation License.
Mercedes Car
This site monitored by SitePinger.net