|
Marekani (inajulikana pia kama "Maungano ya Madola ya Amerika" au kwa kifupi chake cha Kiingereza kama "USA" au "US") ni nchi ya Amerika ya Kaskazini inayopakana na Kanada na Meksiko.
Mji mkuu wa Marekani ni Washington DC.
Eneo
Marekani bara
Eneo la Marekani ni hasa bara la Amerika Kaskazini kati ya Kanada upande wa laskazini na Meksiko upande wa kusini. Marekani imeunganisha upana wote wa bara kutoka Bahari ya Atlantiki na Pasifiki. Marekani bara imegawanywa kwa majimbo 48 yanayojitawala.
Eneo lake lagawiwa katikati na mto mkubwa Mississippi unaoanza mpakani wa Kanada na kuishia katika Ghuba ya Meksiko
Alaska
Jimbo la Alaska liko pia kwenye bara la Amerika Kaskazini upande wa kazkazini ya Kanada ikipakana na Urusi.
Hawaii
Funguvisiwa ya Hawaii ni jimbo la visiwani katika bahari ya Pasifiki.
Visiwa vya ng'ambo vya Marekani
Maeneo ya ng'ambo ya Marekani ni visiwa kadhaa ambavyo ni maeneo ya Kimarekani ingawa si sehemu ya jimbo lolote. Zamani vilikuwa kama koloni hata kama Marekani ilidai kutokuwa na koloni. Siku hizi maeneo haya yamepata viwango mbalimbali vya kujitawala. Kwa kawaida maeneo haya huchagua pia wawakilishi kwa ajili ya bunge la Marekani lakini wawakilishi wale si wabunge wa kawaida wakiwa na haki ya kusema na kushauriana tu bila haki ya kupiga kura.
Visiwa muhimu kati ya hivi ni kama vifuatavyo:
Waja
Tazama pia
 |
Makala hiyo kuhusu "Marekani" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".
Ikiwepo makala kuhusu Marekani kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.
|
|