|
Article on other languages:
|
Puerto Rico ni nchi katika Bahari ya Karibi ambayo ni eneo la kushirikishwa la Marekani katika visiwa vya Antili Kubwa. Iko upande wa mashariki ya Jamhuri ya Dominika na upande wa magharibi ya Visiwa vya Virgin. Jina la Puerto Rico humaanisha "bandari tajiri". Ilikuwa koloni ya Hispania iliyovamiwa na Marekani tar. 25 Julai 1898 wakati wa Vita ya Marekani dhidi Hispania na kutawaliwa kama koloni hadi 1917 ambako watu wa Puerto Rico walipewa uraia wa Marekani na kiwango cha utawala wa mambo ya ndani. Tangu 1948 gavana imechaguliwa na watu si kuteuliwa tena na rais wa Marekani. Funguvisiwa ya Puerto Rico inajumuisha kisiwa kikuu cha Puerto Rico pamoja na visiwa na funguvisiwa vidogo kama vile Mona, Vieques, Monito, Desecheo, Caja de Muertos, Pajaros, Icacos, Palominos, Palominitos, Culebrita, na Culebra. Puerto Rico si jimbo kamili ya Marekani bali nchi inayojitawala katika mambo ya ndani ilhali siasa ya nje na mambo ya uchumi hutawaliwa na Marekani. Wakazi ni raia wa Marekani lakini hawashiriki katika uchaguzi wa rais. Kuna mwakilishi wa Puerto Rico katika bunge la Washington lakini hapigi kura. Watu wa Puerto Rico humchagua Gavana na wabunge wao. Katika kura za 1967 na 1993 walikataa kutafuta uhuru lakini walikataa pia kuwa jimbo kamili la Marekani wakapendelea hali ya eneo la kushirikishwa. Questions for article: all private english schools in luquillo, puerto rico, プエルトリコ tren urbano/urban train, jose gonzalez silver star puerto rico utuado, juana diaz residents 1886, land puertoriko, luquillo, puerto rico- religious beliefs, luquillo.puerto.rico, portoriko, map, portoriko.tourist, portoryko map, tainos de yauco |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
This article is from Wikipedia. All text is available under the terms of the GNU Free Documentation License.
Mercedes Car
This site monitored by SitePinger.net