1 Taz. #Demografia kwa lugha za kimkoa 2 Eneo lote la Ufaransa pamoja na mikoa ya ng'ambo lakini bila Antaktika. 3 Ufaransa bara pekee (=Ufaransa ya Ulaya) 4 Namba za taasisi ya jiografia ya Ufaransa 5 Kumbukumbu ya ofosi ya ardhi 6 Jamhuri yote ya Kifaransa bila maeneo katika Pasifiki 7 Maeneo ya ng'ambo katika Pasifiki pekee
Ramani ya Ufaransa katika Ulaya
Ufaransa ni nchi ya Ulaya. Mji mkuu ni Paris. Ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Eneo lake ni 674,843 km² na idadi ya wakazi ni 63,044,000.
Ufaransa haina dini rasmi lakini wakazi walio wengi (75%) ni Wakatoliki. Kutokana na uhamiaji kuna pia Waislamu wengi.
Wafaransa wanapenda sana michezo hasa mpira wa miguu.
Ufaransa ilikuwa kati ya nchi zenye makoloni mengi ikasambaza lugha yake kote duniani na kutunza uhusiano wa pekee na nchi nyingine zinazotumia Kifaransa.